
Flash required to play audio. |
- Ee Mungu nguvu yetu
Ilete baraka kwetu
Haki iwe ngao na mlinzi
Na tukae na undugu
Amani na uhuru
Raha tupate na ustawi
- Amkeni ndugu zetu
Tufanye sote bidii
Nasi tujitoe kwa nguvu
Nchi yetu ya Kenya
Tunayoipenda
Tuwe tayari kuilinda
- Na tujenge taifa letu
Ee ndiyo wajibu wetu
Kenya istahili heshima
Tuungane mikono
Pamoja kazini
Kila siku tuwe na shukrani
|